Story by Our Correspondents-
Msemaji wa Serikali Kanali mstaafu Cyrus Oguna amesema serikali inafahamu wazi kwamba gharama ya maisha imepanda na swala hilo limechangiwa na uchache wa nafaka nchini.
Oguna ameshikilia kwamba swala hilo limechangiwa pia na changamoto mbalimbali ikiwemo kushuhudiwa kwa ukame, ujio wa janga la Corona na uharibifu wa mimea shambani iliyochangiwa na mdudu nzige.
Katika mahojiano ya kipekee na kituo cha Radio Kaya kwenye kipindi cha Voroni Enehu, Oguna ameweka wazi kwamba vita vinavyoendelea kushuhudiwa nchini Ukraine vinazidi kuchangia kupanda kwa gharama ya maisha kwani Kenya ni kati ya mataifa yanayotegemea pakubwa nafaka kutoka taifa la Ukraine na Urusi.
Akigusia swala la mvutano wa kisiasa kati ya Rais Uhuru Kenyatta na Naibu wake William Ruto, Oguna amesema swala hilo ni jambo la kibinafsi huku akipinga madai yalioibuliwa kwamba Mawaziri wamekuwa wakifanya siasa.
Wakati uo huo amewaondolea shaka wananchi kwamba huenda Rais Kenyatta akadinda kuachilia madaraka baada ya uchaguzi mkuu, akisema ni lazima rais amepeyana madaraka hayo kwa kiongozi atayechaguliwa kwa mujibu wa muongozo wa Katiba.