Story by Our Correspondents –
Msemaji wa serikali Kanali mstaafu Cyrus Oguna amesema serikali imetanga shilingi bilioni 2.4 kununua chakula cha msaada na kusambazwa katika kaunti 23 ambazo zinakabiliwa na ukame na baa la njaa nchini.
Katika kikao na Wanahabari jijini Nairobi, Oguna amesema chakula hicho kitaanza kusambazwa kuanzia mwezi huu wa Oktoba hadi Novemba mwaka huu kwani Muungano wa Afrika AU umetoa msaada wa shilingi milioni 500 kupiga jeki mpango huo.
Oguna amesema Shirika la mpango wa Chakula duniani WFP pia limetoa fedha zengine kupiga jeki juhudi za serikali katika kuwasaidia wakenya walioathirika na ukame kwa kuwasambazia chakula na maji hadi mashinani.
Wakati uo huo Oguna amesema kaunti ya Garissa, Isiolo, Kitui, Marsabat, Wajir, Samburu na Tana river zimeathirika zaidi na ukame na zimepewa kipau mbele katika mpango huo ili kuwanusuru wananchi.