Story by Janet Shume-
Askari wa serikali ya kaunti ya Kwale wameweka wazi kwamba wameweka mipangilio ya kulinda haki za wanawake wanaofanya biashara katika masoko ya kaunti hiyo.
Kulingana na afisa wa kitengo hicho Douglas Oginda wameweka askari wa kaunti wa kutosha katika maeneo hayo watakaoshughulikia visa vya dhulma dhidi ya wanawake.
Oginda ameeleza kwamba maafisa hao wamepewa mafunzo ya kutosha ya jinsi ya kukabiliana na visa viovu vinavyotendewa wafanyabiashara katika masoko hayo ikiwemo jinsi ya kunakili ushahidi.
Kauli hii inajiri baada ya baadhi ya wafanyabiashara wa kike kutoka masomo mbalimbali kaunti ya Kwale kulalamikia kudhulumiwa katika maeneo yao ya kazi pasi na kupata msaada.