Story by Ali Chete-
Ofisi ya mkurugenzi mkuu wa mashtaka ya umma nchini ODPP imezindua rasmi muongozo wa kutatua kesi za dhulma za jinsia katika kaunti ya Mombasa.
Mkurugenzi mkuu wa mashtaka ya umma nchini Noordin Hajj amesema muongozo huo utasaidia idara ya Mahakama kutatua kesi hizo huku akidai kwamba utachangia pia kuielimisha jamii kuhusu sheria zinazofungamana na maswala hayo.
Akizungumza na Wanahabari mjini Mombasa, Noordin amesema ofisi hiyo imejitayarisha kukabiliana na kesi hizo iwapo zitaripotiwa huku akisema tayari wanashirikiana na taasisi mbalimbali za kisheria kuhakikisha uchaguzi mkuu unazingatia amani.
Ni kauli iliyoungwa mkono na Mwenyekiti wa Mamlaka inayotathmini utendakazi wa polisi nchini IPOA Anne Makori aliyezitaka asisi zote za kiuslaama nchini kuzingatia sheria katika majukumu yao.