Viongozi wa chama cha ODM kaunti ya Kwale, wamesisitiza kuwa chama hicho kitahifadhi kiti cha ubunge wa Msambweni na Malindi, iwapo wabunge Suleiman Dori na Aisha Jumwa watatimuliwa kwenye chama hicho na uchaguzi mdogo kuandaliwa.
Viongozi hao wakiongozwa na Naibu Mwenyekiti wa ODM Kwale Nichola Zani, wameahidi kumuunga mkono mwana siasa Omar Boga.
Mwakilishi wa Kike kaunti ya Kwale Zuleikha Juma, amewakashfu Dori na Jumwa kwa kukiuka sheria za chama hicho kwa kuunga mkono azimio la Naibu Rais Dakta William Ruto la kuwania kiti cha Urais kwenye uchaguzi wa mwaka wa 2022.
Naye mjumbe maalum katika bunge la kaunti ya Kwale Fatuma Masito, amesema Mbunge wa Malindi Aisha Jumwa, amewadhalilisha wanawake kwa kutumia matamshi ya matusi mbele ya halaiki ya watu na hastahili kuwa kiongozi.
Taarifa na Michael Otieno.