Story by Our Correspondent:
Kiongozi wa upinzani nchini Raila Odinga sasa anasema yuko tayari kushikilia nafasi ya Mwenyekiti wa umoja wa Afrika AU ili kuhakikisha bara la afrika linapiga hatua kiuchumi, uwekezaji na maendeleo.
Odinga amesema amefanya majadiliano ya kina kuhusu nafasi hiyo na juhudi zinazoendelezwa na serikali ya Kenya katika kuhakikisha viongozi wa Afrika wanaunga mkono mpango huo itasaidia pakubwa kwa bara la Afrika kunawiri kupitia raslimali zilizopo Afrika.
Katika kikao na Wanahabari jijini Nairobi, ambacho kimehudhuriwa na aliyekuwa Rais wa Nigeria ambaye pia ni mpatanishi mkuu Olusegun Obasanjo, Odinga amesema amefanya maamuzi ya kina na yuko tayari.
Kwa upande wake Obasanjo, amesema wakati wa nafasi hiyo kuongozwa na mjumbe kutoka kanda ya Afrika mashariki umewadia, akiweka wazi kwamba watu waliowahi kushikilia nafasi za urais ama Waziri mkuu wako na nafasi nzuri katika kuteuliwa kushikilia nafasi hiyo ya Mwenyekiti wa AU.