Story by Our Correspondents-
Mgombea wa urais kupitia Muungano wa Azimio la umoja One Kenya Raila Odinga anatarajiwa kuzuru kaunti ya Mombasa hii leo ili kuendeleza kampeni za muungano huo sawa na kutafuta kura za kuingia Ikulu Agosti 9.
Odinga amepangiwa kufanya kikao maalum mwendo wa asubuhi na baadhi ya viongozi katika kaunti hiyo kabla kuanza msafara wake wa kisiasa katika maeneo mbalimbali ya kaunti ya Mombasa.
Kulingana na Mkurugenzi wa Mawasiliano katika kamati ya kampeni za Odinga Denis Onsarigo, Mwanasiasa huyo anatarajiwa kuhutubia wakaazi wa eneo la Kengeleni, Sabasaba, Changamwe, kabla ya mkutano mkuu wa kisiasa katika eneo la Jomvu kaunti ya Mombasa.
Hata hivyo viongozi wa Muungano hao akiwemo mgombea mwenza wa Odinga, Bi Martha Karua, Gavana wa sasa wa Mombasa Ali Hassan Joho, Mbunge wa Mbvita ambaye analenga kuwania kiti cha ugavana wa Mombasa Abdulswamad Sharrif Nassir miongoni wa viongozi wengine wanatarajiwa kuandamana na Odinga.