Story by: Mimuh Mohamed
Kinara wa Muungano wa Azimio la umoja Raila Odinga ametangaza kwamba tarehe 20 mwezi huu wa Machi kuwa siku ya kitaifa ya mapumziko ili kutoa nafasi kwa wakenya kushiriki maandamano ya muungano huo yatakayofanyika jijini Nairobi.
Akizungumza katika kaunti ya Siaya Odinga amesema hatua hiyo pia itawezesha wafuasi wa Muungano huo ambao hufanya kazi siku za wiki kushirikia maandamano hayo.
Odinga hata hivyo ameshikilia kwamba hawahitaji vurugu wala umwagikaji damu wakati wa maandamano hayo, akisema wataandamana kwa amani kwani maandamano ni ndio njia pekee waliosalia nayo kupigania haki.
Odinga ametoa tangazo hilo baada ya Kinara mwenza Martha Karua, kumrai kutangaza siku ya Jumatatu ya tarehe 20 ya mwezi huu kuwa siku ya mapumziko kwa ajili ya maandamano hayo.
Hata hivyo kulingana na sheria za nchini, mwenye Mamlaka ya kutangaza siku ya mapumziko ya kitaifa ni Waziri wa usalama wa ndani Pekee, na kuchapishwa katika gazeti rasmi la serikali hivyo basi tangazo hilo la Odinga halitambuliki kisheria.