Picha kwa Hisani –
Kinara wa Chama cha ODM Raila Odinga amesema ana ufahamu zaidi kuhusiana na yaliyomo ndani ya ripoti ya Jopokazi la maradhiano nchini BBI.
Odinga amesema punde tu jopokazi la BBI litakapokamilisha ripoti hiyo, maswala yote yaliyomo ndani ya ripoti hiyo yatawekwa wazi kwa wananchi kwani ripoti hiyo ina malengo muhimu kwa wakenya ikiwemo kupiga vita ufisadi.
Akizungumza wakati wa mkutano wa Wanachama cha chama cha ODM katika kaunti ya Machakos, Odinga amewashtumu vikali wanasiasa wanaopinga mchakato wa BBI, akisema ni lazima viongozi wazingatia uadilifu.
Wakati uo huo amewataka wakenya kuisoma kwa kina ripoti hiyo pindi itakapowasilishwa kwa umma ili kuhakikisha wanaiunga mkono kikamilifu.