Picha kwa hisani –
Kinara wa Chama cha ODM Raila Odinga amesema zoezi la kukusanya saini kupitia mchakato wa BBI litaendelea licha ya kufikisha saini hitajika ili kuifanyia marekebisho Katiba.
Akizungumza na Wanahabari, Odinga amesema tayari zaidi ya saini milioni 5.2 zimekusanywa kufikia sasa na kinachosubiriwa ni Tume huru ya uchaguzi na mipaka nchini IEBC kuidhinisha saini hizo.
Odinga amepuuzilia mbali mapendekezo yaliotolewa na Naibu Rais Dkt William Ruto, kuwa kura ya maamuzi inaweza kusubiri hadi mwaka wa 2022 ili maswala tata ambayo hayajajumusisha katika ripoti ya BBI yajumuishwe, akisema kauli ya Ruto imepitwa na wakati.
Wakati uo huo Odinga amesema nakala za saini hizo za BBI inatarajiwa kuwasilisha zote kwa Kamati husika ya zoezi la kukusanya saini, huku akisema mchakato wa kuifanyia marekebisho katiba hautayumbishwa na kiongozi yeyote.