Story by Our Correspondents-
Kinara wa Chama cha ODM Raila Odinga amevunja kimya chake na kukosoa kauli ambazo zimekuwa zikitolewa na wanasiasa humu nchini kwamba uhusiano wake wa karibu wa kisiasa na Rais Uhuru Kenyatta huenda ikawa anatumika kama mradi wa serikali.
Akizungumza katika eneo bunge la Kieni katika kaunti ya Nyeri wakati wa halfa ya mazishi ya Jucinta Wanjiku aliye mamake Naibu Gavana wa kaunti hiyo, Odinga amesema yeye sio mradi wa serikali na tayari ameukwea mlima Kenya bila ya usaidizi wa rais Kenyatta.
Odinga amesema ana malengo ya kubadili uongozi wa taifa hili na kupitia mpango wake wa Azimio la umoja ni lazima wakenya wote waungane kwani kwa kufanya hivyo ndio taifa hili litapiga hatua kimaendeleo.
Kwa upande wake Gavana wa Nakuru Lee Kinyanjui aliyeandamana na Odinga katika halfa hiyo ya mazishi, amesema wakenya watakuwa salama baada ya uchuguzi mkuu iwapo watamuunga mkono Odinga kuingia Ikulu.