Story by Our Correspondents –
Kinara wa chama cha ODM Raila Odinga ameahidi kuimarisha muundo msingi ili kuhakikisha wakenya wanakabiliana na changamoto mbalimbali za maisha.
Akizungumza wakati wa mikutano yake ya kisiasa jijini Nairobi, Odinga amesema taifa hili litabadilika kiuchumi iwapo wananchi watawachagua viongozi walio na malengo ya kuimarisha uchumi wa nchi.
Odinga ameshikilia kwamba hali duni ya uchumi imetokana na mirundiko ya madeni , akisema swala hilo litatatuliwa kupitia ajenda mwafaka zinazofaa kuanzishwa na kuendelewa kote nchini.
Wakati uo huo amehimiza umuhimu wa wakenya kuishi kwa umoja na kuendeleza mshikamano wa jamii, sawia na kujitenga na ukabila au dini, akisema hatua hiyo itachangia taifa hili kuimarika kiuchumi, maendeleo na kushuhudia amani.