Story Our Correspondents –
Kinara wa Chama cha ODM amesema lengo lake kuu ni kuwaunganisha wakenya wote ili taifa hili lishuhudie mshikamano wa jamii na kufanikisha maendeleo hadi mashinani.
Akizungumza katika kaunti ya Kajiado wakati wa mikutano yake ya kisiasa, Odinga amesema tayari ameanzisha mikakati ya kufanya vikao na jamii mbalimbali nchini ili kuhakikisha jamii zinaungana.
Odinga amesema wakati umefika sasa kwa jamii mbalimbali kuungana na kufanikisha ajenda ya amani na mshikamano wa taifa, akihoji kwamba hatua hiyo itachangia taifa hili kushuhudia amani na umoja.
Kwa upande wake Gavana wa Kajiado Joseph Ole Lenku ameahidi kwamba jamii ya Wamasai iko tayari kushirikiana na kiongozi mwenye malengo ya kuwaunganisha wakenya wote kwa kutambua umuhimu wa jamii mbalimbali nchini.