Story by Our Correspondents –
Kinara wa chama cha ODM Raila Odinga amefanya mkutano na wafanyibiashara pamoja na viongozi kutoka mlima Kenya kujadili mikakati ya kufanikisha siasa za mwaka wa 2022.
Katika mkutano huo uliondaliwa jijini Nairobi, Odinga amesema mikakati ya kuinua uchumi wa nchi, uwekezaji na kufanikisha biashara huru ni kati ya mikakati itakayopewa kipau mbele baada ya kuunda serikali
Odinga ameweka wazi kwamba mikakati ya kukabiliana na janga la ukame nchini inafaa kufanikishwa hasa kwa kuhakikisha jamii inavuna maji ya mvua, akisema hatua hiyo ndio itasaidia wananchi kuwa na maji ya kutosha wakati wa kiangazi.
Akigusia swala la usalama wa taifa, Odinga amesema serikali inafaa kutoa ulinzi wa hali ya juu kwa kila mkenya, huku akidai kuwa hatua hiyo itachangia kuimariika kwa uchumi na maendeleo.
Wakati uo huo amesema huu ni wakati mwafaka wa kuwajenga uwezo wanawake ili kuchangia katika kukuwa kwa uchumi wa nchi, maendeleo na uwekezaji na akiishinikiza Tume huru ya uchaguzi na mipaka nchini IEBC kuwajibikia majukumu yake.