Story by: Gabriel Mwaganjoni
Muungano wa Azimio la Umoja chini ya Kinara wake Raila Odinga, umefanya mkutano wa baraza la wananchi katika kaunti ya Kilifi.
Akihutubia wafuasi wa Muungano huo katika kaunti hiyo, Odinga amesema ataendelea kufichua ukweli kuhusu wizi wa kura ya urais kwenye uchaguzi uliopita bila kujali vitisho kutoka kwa rais William Ruto.
Kwa upande wake Kinara mwenza wa Muungano huo Martha Karua amesema upinzani utaendelea kufanya maandamano ya kupinga serikali akiwataka maafisa wa polisi kuwapa ulinzi wa kutosha waandamanaji wa Muungano huo.
Kwa upande wao viongozi wa kaunti ya Kilifi wakiongozwa na seneta wa kaunti hiyo Stewart Madzayo, wameikosoa serikali ya Kenya Kwanza kwa madai kwamba inawapa wakenya ahadi za uongo kila uchao.
Hayo yakijiri aliyekua Gavana wa Meru Kiraitu Murungi amekosoa maandamano ya Azimio ya kushinikiza serikali kupunguza gharama ya maisha akisema maandamano hayo sio suluhu la changamoto zinazowakabili wakenya.