Kinara wa chama cha ODM Raila Odinga ameongoza mkutano wa kupigia upato ripoti ya kufanyia mabadiliko katiba ya nchini BBI katika kaunti ya Kisumu.
Mkutano huo umejumuisha zaidi ya wajumbe 600 kutoka kaunti za Homabay,Migori,Siaya na Kisumu na unatarajiwa kutoa muelekeo wa wanasiasa wa eneo la Nyanza juu ya ripoti hio ya BBI.
Tayari kaunti ya Siaya ilijadili na kuupitisha mswada huo wa BBI,na kaunti ya Homabay inatarajiwa kuanza kujadili mswada huo kuanzia siku ya jumatano juma hili.
Kikao hiki cha Kisumu ambacho Odinga amehutubia kwa Lugha ya Dholuo kinajiri siku moja baada ya kinara huyo wa ODM kumaliza ziara yake ya siku tatu katika kaunti ya Turkana ziara iliyolenga kushinikiza uungwaji mkono wa BBI.