Story by Our Correspondents-
Kinara wa Chama cha ODM Raila Odinga ameweka wazi kwamba uongozi wa chama hicho umeafikia uamuzi wa kumpa Mbunge wa Mvita Abdulswamad Sharrif Nassir tiketi ya chama hicho ili kugombea kiti cha ugavana wa Mombasa
Katika kikao cha pamoja kilichojumuisha viongozi wa chama cha ODM kutoka kaunti ya Mombasa kilichoandaliwa jijini Nairobi Odinga amesema wamefanya mazungumzo ya kina na viongozi hao na kuafikia uamuzi huo.
Akizungumza kuhusu uamuzi huo, Mwanasiasa Suleiman Shahbal ameahidi kumuunga mkono Nassir ili kuhakikisha chama cha ODM kinanyakua kiti cha ugavana wa Mombasa, huku akisema ataendeleza kampeni za Odinga katika ngazi za kitaifa.
Naye Mbunge wa Mvita Abdulswamad Sharrif Nassir ambaye amepewa nafasi hiyo ameahidi kushirikiana na viongozi wa kaunti ya Mombasa sawa na wakaazi ili kuhakikisha chama cha ODM kinashinda viti vyote vya uchaguzi.
Kwa upande wake Seneta wa Mombasa Mohammed Fakii aliyehudhuria kikao hicho awashukuru viongozi hao kwa kuafikia makubaliano hayo na kusisitiza kwamba hatua hiyo itazidi kuonyesha demokrasia ya chama.