Picha kwa Hisani –
Kinara wa Chama cha ODM Raila Odinga ameendeleza kampeni zake za kuipigia debe ripoti ya jopokazi la maradhiano nchini BBI katika kaunti ya Kwale.
Akizungumza baada ya kukutana na viongozi wa chama kule Msambweni, Odinga amesema ripoti ya BBI inalenga kutatua masuala mengi yanayowahusu wakaazi wa eneo la Pwani ikiwemo maswala tata ya ardhi.
Odinga ameweka wazi kuwa ripoti ya Tume ya haki na maridhiano nchini TJRC inayoangazia dhulma za kihistoria pia itajumuishwa katika ripoti ya mwisho ya BBI.
Akigusia suala la ugavi wa raslimali kwa serikali za kaunti, Odinga amesema iwapo wakenya wataiunga mkono ripoti ya BBI basi maswala ya ugavi wa fedha kwa serikali hizo utakuwa wa asilima 15 hadi 35.
Kauli yake imeungwa mkono na Gavana wa Mombasa Ali Hassan Joho aliyesema BBI ni njia moja wapo ya kuwaunganisha wakenya na suluhu kwa matatizo yanayowakumba wananchi.