Picha kwa Hisani –
Kinara wa chama cha ODM Raila Odinga amekutana na viongozi wa kike wa chama hicho katika eneo la Kitengela jijini Nairobi kuwahamasisha kuhusu masuala mbali mbali ikiwemo yale ya kijinsia.
Odinga amesema chama cha ODM kinalenga kuhakikisha ubaguzi wa kijinsia unaoshuhudiwa nchini unatokomezwa kwa kuhakikisha wanawake,vijana, watoto na wazee wanahusishwa katika masuala muhimu kwa usawa.
Odinga vile vile amesema usawa wa jinsia utaafikiwa humu nchini iwapo jamii mbali mbali katika taifa hili zitaweka kando tamaduni zilizopitwa na wakati na ambazo ni kandamizi.
Katika hotuba yake Odinga vile vile amesema ni lazima taifa liidhinishe mikakati ya kuimarisha uchumi ndipo matatizo mengi yanayokumba wakenya ikiwemo ukosefu wa ajira na umaskini yatakabiliwa.