Picha kwa hisani –
Kinara wa ODM Raila Odinga ameanza rasmi ziara yake ya siku tatu katika kaunti ya Turkana ziara inayojiri siku chache baada ya Rais Uhuru Kenyatta kukamilisha ziara yake ya siku nne katika eneo la kati.
Katika ziara yake ndani ya kaunti hio ya Turkana Odinga anatarajiwa kukutana na viongozi wa chama cha ODM,makundi ya vijana na akina mama pamoja na kuhutubia wananchi wa turkana katika bustani ya Lodwar.
Kinara huyo wa ODM aidha anatarajiwa kuendeleza kampeni za kuipigia upato ripoti ya BBI inayolenga kufanikisha mabadiliko ya katiba.
Tayari Odinga amedokeza kwamba hivi karibu wakenya watapewa nakala za ripoti hio ya BBI ili wapate fursa ya kujisomea kabla ya kushiriki kura ya maamuzi.