Story by Mwahoka Mtsumi –
Kinara wa Chama cha ODM Raila Odinga ameahidi kufanya kazi na Kinara wa chama cha Wiper Stephen Kalonzo Musyoka ili kuhakikisha wanaingia serikalini wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2022.
Akizungumza wakati wa halfa ya Mazishi ya aliyekuwa mbunge wa Kibwezi Richard Kalembe Ndile katika eneo la Mbui Nzau kaunti ya Makueni, Odinga amesema wakati umefika sasa wa kuondoa viongozi tapeli serikalini.
Odinga amesema atashirikiana kikamilifu na Kalonzo ili kuhakikisha wanabuni serikali ya demokrasia wakati wa uchaguzi mkuu ujao sawia na kupigania haki za wakenya waliyonyanyaswa miaka mingi.
Kwa upande waka Kinara wa chama cha Wiper Stephen Kalonzo Musyoka amesema mikakati ya kuchukua uongozi mwaka wa 2022 inaendelea huku akisema mikakati hiyo haitarudi nyuma.
Hata hivyo Mwenzake Kalembe Ndile amezikwa nyumbani kwake katika eneo la Mbui Nzau kaunti ya Makueni.