Story by Our Correspondents –
Kinara wa Chama cha ODM Raila Odinga ameshikilia msimamo wake kwamba analengo la kuwaunganisha wakenya pamoja jinsi alivyoridhiana na Rais Uhuru Kenyatta.
Odinga aliyekuwa akizungumza katika mikutano yake ya kisiasa katika kaunti ya Migori amesema hatua hiyo ndio itakayochangia kushuhudiwa kwa mshikamano wa jamii kupitia mpango wa Azimio la Umoja.
Odinga hata hivyo amesisitiza umuhimu wa wakenya kujitenga na tabia ya ukabila, kidini na maeneo, akisema hatua hiyo haitashuruhusiwa katika serikali yake iwapo wakenya watakamchagua kama rais wa taifa hili mwezi Agosti 9.
Wakati uo huo ameahidi kuboreshwa kwa ugatuzi nchini ili kuwepo na usawa wa ugavi wa raslimali huku akishikilia kauli yake ya kuhakikisha bima ya afya inafikia kila mmoja.