Story by Hussein Mdune-
Mgombea wa kiti cha ubunge wa Likoni kupitia chama Cha UDM Yaq’ub Obado amesema eneo bunge hilo limekosa kushuhudia maendeleo kutokana na uongozi duni.
Akizungumza katika mikutano yake ya kisiasa, Obado amesema tabia ya wakaazi kuwachagua viongozi wasio waadilifu kumesababisha eneo la Likoni kusambaratika kimaendeleo.
Mwanasiasa huyo ameahidi kuwajenga uwezo wafanyibiashara wadogowadogo ili kukabiliana na changamoto za maisha iwapo atachaguliwa wakati wa uchaguzi mkuu wa Agosti 9.