Picha kwa hisani –
Zoezi la usajili wa makurutu wa kujiunga na kikosi cha jeshi lililoandaliwa hii leo katika uwanja wa vigurungani huko kinango kaunti ya Kwale limetibuka,baada ya nyuki kuvamia uwanja huo.
Mmoja wa maafisa wakuu wanaosimamia zoezi hilo Michael Kisingu uvamizi wa nyuki umelemaza zoezi hilo ikizingatiwa kwamba baadhi ya makurutu wamekimbilia usalama wao na huenda wasirejee tena kushiriki zoezi hilo.
Kisingu aidha amesema kuwa baadhi ya watu waliokua wamehudhuria zoezi hilo wamepata majeraha kufuatia mganyagano wakati wakikimbilia usalama wao.