Msanii tajika Nyota Ndogo ametangaza rasmi kuwa anatafuta wachezaji vyombo chipukizi.
Kulingana na msanii huyo anatafuta wasanii watatu. Mchezaji gita la besi, mchezaji ngoma na mchezaji gita.
Nyota Ndogo ameeleza kuwa anatafuta chipukizi ili awakuze kwani anapofanya kazi na wasanii waliobobea huwa wanaleta shida katika kazi hali ambayo haipendelei kama msanii.
“Natafuta mcheza gitaa chipukizi ambae hayupo kwenye bendi yeyote na hana kazi.. Pia natafuta mcheza drums hivyo hivyo na bezi gitaa poa.nataka niwachukue niwakodishie nyumba karibu na Mimi tufanye mazoezi nyimbo zangu mpaka tushikane vizuri.bendi ya watu watatu nirahisi kuisafirisha hata ulaya ukiwa na show ama zile festival Mimi Utanya.sometimes ukichukua ambao washakua wanakuonyesha vile Mimi nishachea huyu Mimi nishachezea yule na mapozi mengi so naitaji kuwakuza hawa kuanzia chini.”
Taarifa na Dominick Mwambui.