Picha Kwa Hisani
Mwanamuziki kutoka Pwani Nyota Ndogo amemwandikia mume wake Hunning Neilsen ujumbe kwenye ukurasa wake wa Instagram akimwomba amsamehe.
Hii ni baada ya mume wake kumkasirikia na kukata mawasiliano kwa muda wa mwezi na nusu sasa.
Kulingana na msanii huyo, hajaweza kuwasiliana na Hunning tangu siku ya April Fools alipomfanyia mzaha. Nyota amedai kuwa amemkosa sana na kama hatorudi basi hatojihuisha na mwanamume mwingine.
“Plzz come back to me. mimi hata sio pesa nalilia love. Nilikua na act don’t care couse nakula nalala vizuri najilipia bills zangu mwenyewe but one thing nakosa from you ni love. Kumbe pesa sio kila kitu muimu kupata mtu unaempenda na wewe kwako nimefika mwisho yani kama hurudi ntajifia single” aliandika Nyota Ndogo.
Nyota alieleza kuwa alimfanyia mzaha kuwa amenasa mimba, jambo ambalo lilimpelekea mume wake kukata simu kasha kumblock.
“Yani nilimwambia nipo na mimba akakata simu toka tarehe moja mpaka Leo. Amenibluetik mpaka mwisho nimekula block. April fools imenikosti. Naenda maliza mwezi sijaskia sauti yake” alieleza Nyota.
Unalizungumziaje swala hili?