Msanii Nyota Ndogo sio mgeni katika kusema ukweli wa jinsi ulivyo.
Katika hulka yake hiyo kupitia ukurasa wake wa Instagram amempa msomo mwanawe wa kiume kwa jina Mbaruk.
Nyota ambaye alirudi hivi majuzi humu nchini kutoka Denmark amemshauri mwanawe kutumia mpira wakati wote atakaposhiriki katika ngono anapokuwa kijana.
Nyota katika usemi huo amekiri kuwa mwanawe amekuwa mkubwa na hawwezi tena kumkataza kuwa na marafiki wa kike lakini akasisitiza umuhimu wa utumizi wa mpira wa kondomu.
Je unakubaliana na ushauri kwa vijana kutumia kondomu?
Taarifa na Dominick Mwambui.