Msanii Nyota Ndogo amekuwa kimya kwa muda mrefu katika tasnia ya mziki humu nchini lakini kama wasemavyo kimya Kingi kina mshindo.
Ukweli wa mambo ni kuwa msanii huyo amekuwa akijihusisha na mziki nchini Denmark na kwa sasa anashughulikia video ya moja kati ya nyimbo alizozifanya akiwa huko.
Kupitia kwa ukurasa wake wa Facebook na Instagram Nyota amekuwa akiachia picha na vipande vya video vya kazi hiyo mpya.
Taarifa na Dominick Mwambui.