Mamlaka ya kudhibiti uchukuzi na usalama nchini NTSA imeombwa kushirikiana vyema na shule za udereva katika kuhamasisha madereva kuhusiana na Rasimu ya masomo mapya ya udereva kabila ya mfumo huo kuanzishwa kutekelezwa rasmi.
Kulingana na mwenyekiti wa shule za udereva ukanda wa Pwani John Magara amesema kwamba idadi kubwa ya maderava nchini hawanaufahamu kuhusiana na masomo mapya huku akisema tayari sheria za Rasimu hiyo zilikuwa zinatumika bararbarai hatua aliyoitaja kupelekea changamato kwa madereva.
Akiongea kwenye warsha iliyowaleta pamoja wadau wa NTSA na wamiliki wa shule za udereva ukanda wa pwani magara amesema kama viongozi hawataruhusu kamwe rasimu hiyo kutumika kama sheria mpaka pale mamlaka hiyo itakapopata maoni mwafaka kutoka kwa wadau wa sekta hiyo.
Kwa upande wake Naibu mkurugenzi kwenye kitengo cha usalama wa barabarani ndani ya mamlaka hiyo Duncan Kibogong Cheriyot NTSA imekanusha madai kwamba Rasimu ya masomo mapya ya udereva haujulikani kwani amesema tayari wameanzisha zoezi la kukusanya maoni kutoka kwa wadau wa shule za uderava nchini.
Taarifa na Hussein Mdune.