Picha kwa Hisani –
Idara ya polisi kaunti ya Kwale imesema zaidi ya watu 200 kutoka kaunti hiyo wamepoteza maisha yao kufuatia ajali za barabarani zinazoendelea kushuhudiwa.
Kamanda wa polisi kaunti hiyo Josepth Nthenge, amesema idadi hiyo imechangiwa na tabia ya wahudumu wa magari ya uchukuzi wa umma kutozingatia sheria za trafiki.
Nthenge amewataka madereva wa matatu, Tuk tuk na bodaboda kuwa waangalifu zaidi wanapokuwa barabarani ili kuepuka ajali.
Wakati uo huo amewaonya madereva dhidi ya tabia ya kukiuka kanuni za afya, akisema ni lazima masharti ya kujikinga na maambukizi ya Corona kuzingatiwa.