Story by Ali Chete
Ushirikiano wa mashirika ya kijamii pamoja na idara mbalimbali za kiserikali umepunguza pakubwa visa vya unyanyasaji wa haki pamoja na utekajinyara wa watu kihohela humu nchini.
Ni kauli iliyotolewa na Mkurugenzi wa mashtaka ya umma Noordin Hajj aliysema tangu ofisi yake ianze kushirikiana na mashirika ya utetezi wa haki za kibinadamu visa hivyo vimepungua pakubwa na kuchangia kupungua kwa magenge ya kihalifu.
Akizungumza mjini Mombasa, Noordin amesema tangu ushirikiano huo uanze visa vya kihalifu vimepungua kwa asilimai 70 huku vile vya watu kupotezwa katika hali tatanishi vikipungua kwa asilimia 20.
Wakati uo huo amedokeza kwamba swala la uhalifu husababishwa na kuchaguliwa kwa viongozi wasiowajibika na waliokosa maadili.