Kamati ya bunge la kitaifa inayaohusika na maswla ya mchezo,utamaduni na utalii wameita wizara ya ardhi nchini kuhakikisha kwamba ardhi zilizonyakuliwa kwenye bustani ya Mama Ngina mjini mombasa zimerudishwa .
Wakiongea wakati walipozuru eneo hilo kuthathimini mradi wa kiurembesha bustani hiyo mwenyekiti wa kamanti hiyo Victor Munyaka amesema kuwa kuna haja ya ardhi zilizonyakuliwa kurudishwa mara moja ilikuona kwamba hazitatizi ujenzi wa mradi huo.
Aidha amemtaka mwanakandarasi mwenye alipewa ujenzi wa maradi huo kutekeleza majukumu yake kwa haraka sawia na kufanya mradi huo kuwa bora zaidi.
Kwa upande wake waziri wa utalii nchini Najib Balala amesema tayari wako kwenye mazungumzo na wizara ya ardhi Kuhusiana na kurudishwa kwa ardhi hizo huku akisema ardhi ya mamangina ni ya serikali na hawataruhusu kamwe visa vya unyakuzi wa ardhi ndanii ya bustani hiyo.
Hata hivyo amesema kuwa shughuli za kurembesha bustani hiyo zimefikia asilimia 45 na wanatarajia mradi huo kukamilika kufikia tarehe 30 mwezi wa Sita mwakani huku akisema shughuli hiyo itagharimu shilingi milioni 460.
Taarifa na Hussein Mdune.