Tume ya kitaifa ya ardhi imesema kuwa itafutilia mbali hati miliki zote za watu wanaomiliki vipande vya ardhi katika shamba la serikali la ADC lilioko eneo la Malindi kaunti ya Kilifi.
Katika mahojiano ya kipekee na Radio Kaya mwenyekiti wa tume hio Dkt Mohamed Swazuri amesema kuwa tayari ametoa notisi ya kutekelezwa kwa suala hilo.
Swazuri aidha ameweka wazi kwamba iwapo hatimiliki za wanaomiliki ardhi katika shamba hilo la ADC zitafutiliwa mbali, shamba hilo halitogawanywa kwa wananchi kama wanavyotarajia wakaazi.
Taarifa na Mimuh Mohamed.