Mwanamuziki kwa jina Nusra Mwatela,anayejulikana kwa jina la stage kama Nizzy Monteh kutoka Ukunda, aliyetamba kwa nyimbo zake za mtindo wa Ragga, Songa na Jibambe sasa ameweka wazi kuwa anaamini kuwa mambo yatakuwa moto zaidi chini ya Lebo mpya ya Lights Records ya Prodiuza mkali zaidi mkoani Pwani anayetamba kwa jina la Prodiuza Ink, baada ya kuwapa mkono wa buriani wahusika na prodiuza wa Blue Star Records.
Nizzy Pia amedokeza kuwa uamuzi wake wa kujiunga na Ink,ni uamuzi mzuri sana kwani anafahamu kuwa amejiunga na simba wa kutayarisha muziki mzuri. Prodiuza Ink aliwahi kufanya kazi na wasanii wakubwa mkoani Pwani wanaovuma hata nchi jirani. Mmoja wa wasanii hao wanaofanya kazi chini ya Ink,ni msanii anayekwenda kwa jina la Amarila,aliyeimba wimbo mkali kwa jina Twafanana, https://www.youtube.com/results?search_query=twafanana
Nizzy pia amekishukuru kituo cha Radio Kaya kwa kumpa support na kucheza muziki wake na hatimaye kuongoza chart ya ngoma 5 kali zaidi mkoani Pwani. Je,siri ya haya yote ni nini? “Hakuna kingine zaidi ya kujieshimu na kueshimu pia na watu wengine,pia licha ya kuwa mimi ni msichana mwenye mvuto kwa kila mwanamume,basi lazima kujieshimu ndo maana niko vizuri na naamini bado nitaendelea kuwa vizuri zaidi” Nizzy alikiri. Je,kwa nini uliamua kuachana na studio za Blue Star Records? “aaaaah,bado ni mapema sana kwa kueka wazi ama kukuelezea kwa kiundani sababu zilizonishawishi mimi kufanya uamuzi huo”…..”cha muhimu naomba tu mashabiki wangu wawe mkao wa kula,kwa kuwa kuna kitu kinakuja na nimatumaini yangu kuwa kinachokuja ni kitu kizito zaidi, chini ya Prodiuza Ink wa Lights Records”
Tunatarajia kitu kizito kutoka kwa mkali wa mauno, Nizzy Monteh….
Kwa burudani zaidi tegea Radio Kaya
On air direct line – 0702 931931 // 0702 997997 // 0702 949949 // 0702 885885
SMS – 20931
Facebook – @Radiokaya
Twitter – @RadioKaya
Instagram – @RadioKaya
Online – www.radiokaya.co.ke