Siku zote wanasema mwanzo wa kitu ndio mgumu zaidi. Nayo safari ya mziki yaJosepg Ngala maarufu kama Mzee Ngala Mwenyewe haikuwa rahisi kama wengi wanavyodhania.
Kulingana naye alianza kwa kuchoza “Firimbi” yaani flute alipokuwa katika shule ya upili ya Shimo La Tewa mwaka wa 1954.
Ilimchukua miaka miwili zaidi ili kuanza kutumia vifaa vya kisawa vya mziki.
“Mziki nilianza kwa tabu sana. Mwanzo hatukuwa na vifaa vya kucheza. nilipokuwa shule nilikuwa nikicheza flute. Firimbi ya tundu sita ile,” amesea Mzee Ngala kwenye makala kwa jina Longa Longa yanayoendelea katika mtandao wa youtube kwenye chaneli ya Radio Kaya.
Taarifa na Dominick Mwambui.