Picha kwa hisani –
Watu wenye silaha wamemuua mwanafunzi mmoja na kuwateka nyara wengine 27 katika uvamizi dhidi ya shule yao ya kulala katika eneo la kati, kaskazini mwa Nigeria, amesema gavana Abubakar Sani Bello.
Wafanyakazi wa shule watatu na ndugu zao 12 pia wametekwa nyara katika tukio hilo lililotokea usiku.
Vikosi vya usalama vimepelekwa kusaidia katika shughuli za uokozi.
Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari ameamrisha vikosi vya nchi hiyo kufanya kila liwezekanalo kuwanusuru waliotekwa.
Jumatatu watu wapatao 20 waliokuwa njiani wakitoka katika sherehe za harusi walitekwa nyara wakati basi lao liliposhambuliwa katika jimbo la Niger.
Mwezi Disemba zaidi ya wanafunzi 300 wavulana walitekwa katika mji wa Kankara uliopo katika jimbo la kaskazini-magharibi la Katsina. Baadae waliachiliwa huru baada ya mazungumzo na watekaji wao.