Picha kwa hisani –
Kamanda wa polisi katika jimbo la Kano Kaskazini mwa Nigeria amethibitisha kifo cha Mustapha Muhammad, mkazi wa kijiji cha Malam Na Andi, ambaye amedaiwa kujiua kwa chupa.
Polisi wamesema mwanaume huyo aliamua kujiua kwa njia hiyo baada ya kujifungia ndani ya nyumba katika eneo la Masukwani katika jimbo la Kano ambapo alipanda kwenye dirisha la nyumba yake, kabla ya kukata sehemu zake za siri.
Msemaji wa polisi katika jimbo la Kano Haruna Kiyawa amesema walipokea ripoti kuwa kijana alikuwa amejifungia ndani ya nyumba katika eneo la Musukwani huku akiwa na chupa mkononi mwake.
Kiyawa aliongeza kuwa kijana huyo aliingia ndani ya chumba na kukata uume wake na kujidunga kwa chupa aliokuwa ameivunja upande mmoja katika maeneo mbalimbali ya mwili wake.
Usman Umar, mmoja wa marafiki wa marehemu, amesema kuwa alimsikia marehemu akiongea na mtu ambaye hakuonekana, saa kadhaa kabla ya kujiua, huku akiwa amevaa kaptula huku akizozana na mwanaume mwingine lakini hakumuona.
Ibrahim Abdusallam, kaka yake mdogo wa marehemu Mustapha, pia amesema mwendazake alikuwa na ugonjwa wa akili wakati mmoja alipotoka Saudi Arabia, na siku tatu kabla ya kifo chake maradhi yalikuwa yamerejea na alikua katika hali mbaya zaidi.