Picha Kwa Hisani.
Nicki Minaj amempongeza muimbaji nyota wa muziki wa RnB Rihanna baada ya taarifa kwamba yeye pamoja na mpenzi wake ASAP wanatarajia mtoto wao wa kwanza kusambaa kote ulimwenguni.
Jana picha za Rihanna mwenye umri wa miaka 33, zinazoonyesha ujauzito wake zilisambaa kwenye mitandao mbali mbali ya kijamii huku msanii huyo akitrendi nambari moja kwenye mtandao wa twitter.
Picha Kwa Hisani.
Katika picha hizo, zilizopigwa jijini New York mwishoni mwa wiki na kuchapishwa Jumatatu, Januari 31, Rihanna anaonekana akionesha tumbo lake huku A$AP akimbusu kwnye paji la uso.
Habari hii ya ujauzito inakuja miaka miwili baada ya wawili hao kuhusishwa na taarifa kuwa ni wapenzi, tetesi zilizokuwepo muda mfupi baada ya kutengana na Hassan Jameel.
Uhusiano ulianza baada ya nyota hao kuonekana wakiwa pamoja huko New York.
Picha Kwa Hisani – Nicki Minaj.
Aliyekuwa rafiki yake wa karibu, Nicki minaji hajasazwa na habari hizi huku akijitokeza na kumpongeza Rihanna kwa mimba yake.
Nicki alitumia ukurasa wake wa instagram, kuchapisha picha iliyokuwa ikionyesha mimba ya Rihanna iliyoambatana na maneno ya kumpongeza na kumkaribisha kwa hatua nyingine ya maisha.
Picha Kwa Hisani – Rihanna.
Rihanna alipakua picha ya ujauzito wake wakiwa na mpenzi wake A$AP Rocky, pia mwenye umri wa miaka 33, ambaye alitajwa kuwa na furaha kubwa anapotarajia kifungua mimba.