Picha kwa Hisani
Rapper wa kike kutokea Marekani Nicki Minaj amefichua kuwa ni mjamzito na anatarajia kujifungua hivi karibuni. Nicki ambaye ana umri wa miaka 37 alichapisha picha zinazomuonesha kuwa mjamzito kupitia ukurasa wake wa instagram.
Nicki Minaj Hii ni miezi michache baada ya rapper huyo kutangaza kuwacha muziki ili kushughulikia ndoa na familia yake. Licha ya kuwa kwenye mahusiano tofauti tofauti lakini hakuwahi kuwa na mtoto hivyo huyu ndiyo atakuwa mtoto wake wa kwanza.
Nicki pia alieleza furaha yake katika ndoa na upendo anaoonyeshwa na mume wake haswa katika kipindi cha uja uzito wake.
Mashabiki na wanamuziki wenzake wamempa hongera kwa kumpost kwenye mitandao tofauti tofauti ya kijamii.