Story by Gabriel Mwaganjoni-
Baraza la Wazee wa Mijikenda katika kaunti ya Mombasa limemuidhinisha Mwaniaji wa kiti cha Wadi ya Bamburi Caleb Ngwena kama watakayemuunga mkono katika kinyang’anyiro hicho.
Wazee hao wamemtawaza Mwanaharakati huyo wa kutetea haki za binadamu wakisema anastahili kunyakua uwakilishi Wadi ya Bamburi kwani eneo hilo limetengwa kimaendeleo.
Wakiongozwa na Mzee Karisa Kadenge Malingi, Wazee hao wamemtaka Ngwena kuyaangazia maslahi yao ya kimsingi pindi atakapoingia katika bunge la kaunti ya Mombasa.
Kwa upande wake, Ngwena ameapa kubuni Baraza la wazee watakaompatia mwelekeo katika utendakazi wake mashinani.