Tume ya uwiano na utangamano wa kitaifa NCIC imewataka wazazi katika kaunti ya Kwale kuwajibikia majukumu yao ya ulezi kwa kufuatilia mienendo ya watoto wao ili wasiangamie.
Afisa mkuu mtendaji wa tume hiyo Mohamed Hassan amesema kuwa idadi kubwa ya wazazi katika kaunti ya Kwale wamezembea katika kuwalea watoto wao na kuwaachilia kurandaranda mtaani.
Afisa huyo amesema kuwa idadi kubwa ya watoto walio chini ya umri wa miaka 18, wamejiunga na magenge ya uhalifu kaunti ya Kwale kutokana na uzembe wa wazazi kwenye masuala ya ulezi.
Amewahimiza wazazi kuchukulia kwa uzito maadili ya watoto wao iwapo wanataka wawe na maisha bora katika jamii siku za usoni.
Taarifa na Michael Otieno.