Picha kwa hisani –
Tume ya uwiano na utangamano wa kitaifa nchini NCIC imewataka wafanyikazi wa serikali kutojihusisha na masuala ya siasa na badala yake watuwajibikie majukumu waliokabidhiwa.
Akizungumza na wanahabari mapema leo kamishna wa tume hio Sam Kona amesema hatua hio imepelekea viongozi kurushiana cheche za maneno na kuchochea mgawanyiko miongoni mwa wakenya.
Kona amemtaka kiongozi wa nchini Uhuru Kenyatta kutoa onyo kwa maafisa wa serikalini ikiwemo mawaziri kutoendeleza siasa akisema tume ya NCIC iko macho kuwafatilia viongozi wanaotoa matamshi ya uchochezi.
Kamishna huyo wa NCIC amesema tume hio inafanya kazi bila upendeleo na kwamba kiongozi atakaetoa semi tatanishi na zinazolenga kuchochea wakenya ataadhibiwa bila kujali cheo chake.