Tume ya uiano na utangamano wa kitaifa NCIC imeanzisha hamasa kwa vijana wa kaunti ya Kilifi kama njia moja wapo ya kuleta amani na kupiga vita swala la itikadi kali.
Mkurugenzi Mkuu wa tume hiyo Hassan Muhammed amesema kuna haja ya vijana kuhamaishwa jinsi ya kudumisha amani na kusitisha mauaji ya wazee kiholela kwa tuhma za uchiwi katika kaunti hiyo.
Akizungumza na Wanahabari baada ya kikao hicho cha hamasa kule mjini Kilifi, Hassan amewataka vijana kuwa na uvumilivu na kujibunia ajira.
Kwa upande wao vijana hao, wakiongozwa na Asili Randani wameitaka tume hiyo kuwahusisha kikamilfu viongozi wa kidini katika suala la amani na kutoa wito kwa serikali ya kaunti hiyo kuibuka na mikakati ya kukabiliana na itikadi kali.
Taarifa na Marieta Anzazi.