Picha kwa Hisani –
Aliyekuwa kamishna wa tume ya uwiano na utangamano wa kitaifa NCIC Prof Gitiel Naituli amesema ili tume hio kuwa na makali ni lazima kuteuliwe makamishana ambao hawatokubali kutumiwa vibaya na wanasiasa.
Naitula amesema tume hio imeshutumiwa kutowajibikia majukumu yake kutokana na hatua ya makamishna wake kutokua na misimamo dhabiti ya kupigania uwiano wa taifa na badala yake kushirikiana na viongozi wanaoendeleza mgawanyiko.
Akizungumza na wanahabari Naitula amesema NCIC kwa sasa inapaswa kupewa fedha zaidi za kuiwezesha kuendeleza hamasa wananchi kuhusu jinsi wanavyoweza kusimama kwa umoja licha ya wanasiasa kutofautiana.
Kauli yake imejiri siku moja baada ya kushuhudiwa machafuko katika eneo la Kenol,huko Murang’a kati ya wafuasi wa naibu rais William Ruto maarufu tangatanga na wafuasi wa upande wa kieleweke na kupelekea vifo vya watu wawili.