Story by Gabriel Mwaganjoni
Mgombea wa kiti cha ugavana wa kaunti ya Mombasa Abdulswamad Sharif Nassir amewarai wakaazi wa kaunti hiyo ambao walijiondoa katika mrengo wa Azimio na kushirikiana na mirengo mingine ya kisiasa kurudi katika mrengo huo.
Nassir amesema ni kupitia ushirikiano kati ya wakaazi na viongozi wa kaunti hiyo ndipo utawawezesha wakaazi kupata uongozi bora na kunufaika moja kwa moja kimaendeleo.
Akizungumza katika eneo bunge la Jomvu, Nassir anayewania ugavana wa Mombasa kwa tiketi ya chama cha ODM amewasihi wakaazi wa kaunti hiyo kutohadaiwa na baadhi ya wanasiasa wasiokuwa na agenda ya maendeleo.
Nassir pamoja na mgombea mwenza wake Francis Thoya wamewadhihirishia wakaazi wa kaunti hiyo matumaini ya kunyakua kiti cha ugavana ifikapo Agosti 9.