Story by Gabriel Mwaganjoni –
Mbunge wa Mvita Abdulswamad Shariff Nassir ameshikilia kwamba anatafuta uungwaji mkono na wakaazi wa kaunti ya Mombasa na wala sio kubabaishwa na wale wanaotumia ushawishi wao wa kifedha ili kutafuta umaarufu wa kisiasa.
Nassir amesema baadhi ya wagombea wa Ugavana katika kaunti hiyo wamewekeza katika siasa za utajiri bila ya kufahamu kwamba wakaazi wa kaunti ya Mombasa kwa sasa wanawakagua Viongozi kulingana na maadili na tajriba yao ya maendeleo.
Akizungumza katika eneo bunge lake la Mvita, Nassir amesema hababaishwi na wanasiasa matajiri na badala yake anashirikiana na wakaazi kufanikisha mchakato wa maendeleo ya kaunti ya Mombasa.
Mgombea huyo wa ugavana wa Mombasa katika kinyang’anyiro cha Agosti 9 mwaka 2022, amewarai wakaazi wa kaunti hiyo kuwakagua wanasiasa wote wanaowania nafasi za uongozi ili kujitenga na wanasiasa wasio wajibika.