Story by Gabriel Mwaganjoni –
Mbunge wa Mvita Abdulswamad Sharif Nassir amewarai wakaazi wa kaunti ya Mombasa kuwakagua wagombea wa nyadhfa mbalimbali za uongozi katika uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2022.
Nassir amesema ni jukumu la wakaazi kuwachagua viongozi wawajibikaji pekee watakaobadilisha hali yao ya maisha na wala sio wale wanaotumia ushawishi wao wa kifedha ili kununua kura.
Akizungumza katika eneo la Jomvu kaunti ya Mombasa, Nassir amesema ni sharti wakaazi waelimishwe kuhusu swala la uongozi ili wafahamu jinsi ya kuwachagua viongozi waadilifu na wala sio kuhadaiwa kifedha na kuwaweka mamlakani walaghai.
Nassir hata hivyo amewasihi wakaazi wa kaunti hiyo kumuunga mkono katika azma yake ya kuwania nyakua ugavana wa Kaunti hiyo ya Mombasa.