Story by Gabriel Mwaganjoni –
Mbunge wa Mvita Abdulswamad Shariff Nassir amelirudisha tena bungeni swala la kubadilishwa kwa sheria inayosimamia mali ya Waislamu chini ya Tume ya Waqfu ili sheria hiyo iambatane na katiba.
Nassir amesema sheria inayotumika kwa sasa imepitwa na wakati huku baadhi ya mali iliyowekwa chini ya Waqfu huo ikikosa kuwanufaisha wenyewe, huku wamiliki wengine wakiwa tayari walifariki.
Nassir amesema ni sharti maadili na misingi ya dini ya Kiislamu ifuatiwe kikamilifu na sheria hiyo inastahili kupigwa msasa.
Wakati uo huo, Nassir amesema sheria hiyo inatoa nafasi ya kuteuliwa kwa makamishna walio na tajriba na watakaotuma maombi na kusailiwa kabla ya kukabidhiwa majukumu ya kusimamia mali hiyo ya jamii ya Kiislamu.