Story by Gabriel Mwaganjoni-
Mwaniaji wa Ugavana wa kaunti ya Mombasa kwa tiketi ya chama cha ODM Abdulswamad Sharif Nassir ameitaka taasisi ya bandari kuwekwa vifaa hitajika ili kuboresha mafunzo ya ubaharia nchini.
Nassir vile vile ameitaka Serikali kukamilisha ujenzi wa chuo cha utalii cha Ronald Ngala katika kaunti ya Kilifi ili chuo hicho kiwe na sekta maalum itakayotoa mafunzo ya ubaharia na kuwakimu wakaazi wa Pwani.
Akizungumza alipokutana na mabaharia katika kaunti ya Mombasa, Nassir ameitaja kama aibu kwa mabaharia wa humu nchini kulazimika kusafiri hadi ughaibuni ili kupata mafunzo ambayo wangeyapata humu nchini kwa gharama ya chini.
Mwanasiasa huyo hata hivyo ameahidi kushinikiza kutekelezwa kwa matakwa hayo na kutambuliwa kwa sekta ya ubaharia nchini ili iwakimu mamia ya vijana wa Pwani kwa ujuzi utakaowawezesha kunufaika na sekta ya uchumi samawati yaani Blue Economy