Story by Gabriel Mwaganjoni-
Wakaazi wanaoishi katika nyumba za ‘New flats’ eneo la Changamwe katika kaunti ya Mombasa wanahofia kutimuliwa kwenye nyumba hizo baada ya Shirika linalomiliki nyumba hizo kuanza kuzizingira ukuta.
Nyumba hizo chini ya mpango wa makaazi ya kitaifa wa ‘National housing’, zimekabiliwa na mgogoro kati ya wakaazi na mmiliki wake yapata miaka 10 sasa bila ya kuwepo na mwafaka wowote.
Wakiongozwa na mmoja wa wakaazi wa nyumba hizo Josephine Keno, wakaazi hao wamesema wamekuwa wakilipa kodi ya kila mwezi kwa miaka zaidi ya 50 huku Shirika hilo likiapa kuwatimua bila ya majadiliano yoyote.
Kwa upande wao, mgombea wa ugavana katika kaunti ya Mombasa kwa tiketi ya Chama cha ODM Abdulswamad Sharif Nassir na mgombea mwenza wake Francis Thoya wameapa kuingilia kati swala hilo.